Pages

Sunday, November 3, 2013

TAZAMA PICHA JINSI CLUB MAISHA DODOMA WALIPOZINDUA DJ LIVE DRUMMER


Zungu Myama awa kivutio kikubwa sana ndani ya New Maisha club siku ya jana:
Kikosi cha xtreme Jeejayz ambacho hakika kila kukicha kinazidi kujijengea heshima kubwa ndani ya nchi na nje ya nchi kwa ubunifu mkubwa wanaoufanya wa kutoa burudani zenye utofauti na zinazotolewa mahara pengine.
Tarehe 2/11/2013 jana Xtreme Deejayz walikuwa na onesho maalum na utambulisho wa staili yao mpya ya DJ LIVE DRUMMER ambayo imezinduliwa mapema mwezi uliopita Jijini Dar kwenye Club Maisha.

Mwandishi wetu alishuhudia vijana hao wa Xtreme Deejayz wakiongozwa na Dj mkongwe nchini Dj Majey Majizo 4 Chizo ambae pia ndiye mkurugenzi mtendaji wa Club Maisha zote nchini ambapo onesho hilo lilifanya hakuna mfano na kuwachanganya mashabiki kiasi cha kushindwa kuamini kama mambo yaliyokuwa yanafanyika ni ya watanzania au laa.
Shoo hiyo ilianza saa sabana na dakika 20 za usiku ambapo Dvj  Majey, Zungu Mnyama na Hyperman Hk walianza kutoa burudani kwa mashabiki waliokuwa wamejazana wanaokadiliwa kufikia zaidi ya elfu mbili mia tano huku Zungu akicharaza drum kama hana akili nzuri.

Hata hivyo katika hali isiyotegemewa mashabiki wengi walionekana kukunwa vilivyo na Zungu Mnyama ambae ni mlemavu wa ngozi lakini alionesha kipaji cha hali ya juu kiasi cha kuwaliza baadhi ya mashabiki huku wakijikuta wakimwagia mihela kibao kama kuonesha upendo wao kwao huku wengine wakitoa machozi yao.









Aidha katika hatua nyingine mashabiki wengi waliridhishwa na show hiyo hadi kuuomba uongozi wa Club hiyo kuandaa kila wiki  ili waweze kupta burudani ya namna hiyo.

No comments:

Post a Comment