PICHA HAPO CHINI NI YALIYOJIRI KATIKA BONANZA LILILOKUWA LIKIENDELEA CHUONI HAPO AMBAPO FINAL CHUO CHA ST JOHN KILIIBUKA KIDEDEA KWA KUIBUKA NA USHINDI: |
Monday, November 11, 2013
HAYA NDO YALIYOJIRI UDOM KATIKA PARTY YA WELCOME 1ST YEAR BASH, ILIKUWA NI BALAA:
Sunday, November 3, 2013
TAZAMA PICHA JINSI CLUB MAISHA DODOMA WALIPOZINDUA DJ LIVE DRUMMER
Mwandishi wetu alishuhudia vijana hao wa Xtreme Deejayz wakiongozwa na Dj mkongwe nchini Dj Majey Majizo 4 Chizo ambae pia ndiye mkurugenzi mtendaji wa Club Maisha zote nchini ambapo onesho hilo lilifanya hakuna mfano na kuwachanganya mashabiki kiasi cha kushindwa kuamini kama mambo yaliyokuwa yanafanyika ni ya watanzania au laa. Shoo hiyo ilianza saa sabana na dakika 20 za usiku ambapo Dvj Majey, Zungu Mnyama na Hyperman Hk walianza kutoa burudani kwa mashabiki waliokuwa wamejazana wanaokadiliwa kufikia zaidi ya elfu mbili mia tano huku Zungu akicharaza drum kama hana akili nzuri.
Hata hivyo katika hali isiyotegemewa mashabiki wengi walionekana kukunwa vilivyo na Zungu Mnyama ambae ni mlemavu wa ngozi lakini alionesha kipaji cha hali ya juu kiasi cha kuwaliza baadhi ya mashabiki huku wakijikuta wakimwagia mihela kibao kama kuonesha upendo wao kwao huku wengine wakitoa machozi yao.
Aidha katika hatua nyingine mashabiki wengi waliridhishwa na show hiyo hadi kuuomba uongozi wa Club hiyo kuandaa kila wiki ili waweze kupta burudani ya namna hiyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)