Pages

Tuesday, April 29, 2014

FURSA: MAFUNZO YA KUPIGA ALA ZA MUZIKI KUANZA TENA MWEZI MEI‏

 Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mazoezi

Action Music Tanzania (AMTz) inatangaza fursa kwa watu wote kujiunga na mafunzo ya kupiga ala za muziki yanayoanza tarehe 3/5/2014, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wanamuziki wa kupiga ala na kufanya maonesho kwa weledi na utaalamu zaidi.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa darasani

Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na upigaji wa ala za muziki zikiwemo gita, kinanda, tarumbeta, saxophone, konga, drum set, na upigaji wa ngoma za asili. Pia yatatolewa mafunzo ya ‘body percussion’ yaani matumizi ya mwili katika kutengeneza midundo ya muziki.

Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ofisi za AMTZ zilizopo maeneo ya Mwenge mtaa wa Umoja, nyuma ya magorofa ya jeshi na kwenye Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo ili kujiunga na mafunzo haya wasiliana nao kwa simu namba 0686928828/0653075791 ili kupata fomu za kujiunga na mafunzo.

Wednesday, April 16, 2014

Shindano la Tanzania Movie Talents lapokelewa Vyema na Watanzania wa Mikoa ya Mwanza na Dodoma‏

  
Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Dodoma
Watanzania wa Mikoa ya Mwanza na Dodoma wameipongeza kampuni ya Proin Promotions Limited kupitia shindano lao la Kusaka vipaji vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents kwa kuamua kuanzisha shindano hilo ambalo limeanza kuonyesha matumaini kwa vijana wenye vipaji vya kuigiza ambao walisahaulika katika tasnia hiyo ya filamu nchini.
Shindano hili la Tanzania Movie Talents linawawezesha watanzania wote wenye vipaji vya kuigiza kuweza kujitokeza ili kuweza kuonyesha vipaji vyao na kuvikuza kwa kutumia fursa hii iliyoanzishwa na kampuni ya Proin Promotions Limited

Wakiongelea kuhusu shindano hili la Tanzania Movie Talents, wakazi wa Mkoa wa Dodoma walisema" tunafurahishwa sana na shindano hili kuweza kuanzishwa Tanzania na Afrika Mashariki na Kati kwani sasa tunaweza kupata nafasi katika tasnia ya filamu baada ya kuanza kuonyesha vipaji vyetu vya kuigiza"
"Tanzania Movie Talents inamgusa kila mtanzania mwenye vipaji vya kuigiza kwani ni nafasi kwa vijana na watanzania wote wenye vipaji vya kuigiza kuweza kujitokeza kwaajili ya kuonyesha uwezo na vipaji vyao vya kuigiza, Shindano la Tanzania Movie Talents ni mkombozi wa Vijana na watanzania ambao wana vipaji vya kuigiza ambapo kupitia shindano hili vijana wanaweza kupata nafasi za ajira kupitia tasnia ya filamu nchini ambapo washiriki watakuwa wameweza kuonekana na hatimaye kuitwa kwaajili ya kufanya kazi.

Kwa upande wake baadhi ya wafanyakazi wa timu ya Tanzania Movie Talents walithibitisha kuwa 'Tanzania Movie Talents imepokelewa vizuri na watanzania wa Mikoa ya Mwanza na Dodoma  kwani tumeona ongezeko la washiriki waliojitokeza kwaajili ya usaili wa kushiriki katika Shindano hili kubwa na la kwanza Afrika Mashariki na Kati. Hii nikutokana na ukweli kwamba washiriki wote wanaofika kwaajili ya Usaili hawatozwi kiasi chochote cha pesa kutoka timu ya Tanzania Movie Talents na pia kufurahishwa na uamuzi wa Majaji wa Timu ya Tanzania Movie Talents,  niwazi kabisa kuwa kutotozwa kwa kiasi chochote cha pesa kwa washiriki kumekuwa ni kivutio kikubwa kabisa hivyo kuongeza idadi ya washiriki katika kila Kanda tunayoenda"alisema Stephen Mapunda Mkazi wa Mkoa wa Dodoma

Wednesday, April 9, 2014

HAWA NDIO WASHIRIKI WA REDS MISS UDOM 2014, TAZAMA BAADHI YA PICHA WAKIFANYA MZOEZI NEW MAISHA CLUB

Hawa ni ndio washiriki wa Reds Miss Udom 2014 watakaochuana Ijumaa hii ya tar 11 /4/ 2014 katika Ukumbi mpya wa Kilimani Landmark
Warembo hawa  watasindikizwa na kisima cha burudani kutoka kwa wana wa Kutwanga na Kupepeta ambapo timu nzima ya Twanga Pepeta itatoa burudani isiyoyakifani kwa kiingilio cha kawaida cha buku kumi (10,000 )malango na VIP Meza moja ya watu 6 ni shilingi laki moja tu(100,000)
Mazoezi ya Mashindano haya yanafanyika New  Maisha Club Chini ya Dj Abou Mkali kwenye Mashine A.K.A Shemeji,
Na pia katika siku ya kesho Jumatano ya Tar 9 April kutakuwa na Mchujo ambapo warembo kumi watachaguliwa kuingia moja kwa moja kwenye Mchuano huo na siku ya Ijumaa watapanda Jukwaa moja na kumpata mshindi atakayeiwakilisha Udom katika Miss Tanzani 2014

USIKOSA KUSHUHUDIA MCHUANO MKALI WAREMBO KUTOKA UDOM IJUMAA HII KTK UKUMBI WA KILIMANI LANDMARK